Thursday, December 18, 2014

COASTAL UNION YACHEZA SOKA SAFI,MWADUI YAILAZIMISHA SARE MKWAKWANI LEO


KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOLAZIMISHWA SARE NA MWADUI YA SHINYANGA LEO 

WAGOSI WA KAYA WAKIPIGA DUA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO.
KIKOSI CHA TIMU YA MWADUI YA SHINYANGA KILICHOCHEZA NA COASTAL UNION LEO

KUSHOTO NI KOCHA MKUU WA COASTAL UNION  JAMES NANDWA AKIBADILISHANA MAWAZO NA MKURUGENZI WA BENCHI LA UFUNDI COASTAL UNION MOHAMED KAMPIRA KABLA YA KUANZA MECHI YA KIRAFIKI KATI YA COASTAL UNION NA MWADUI YA SHINYANGA.
KUTOKA KULIA NI MENEJA WA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI,KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI WAKIFUATILIA MCHEZO WA LEO WAKIWA SAMBAMBA NA MASHABIKI WENGINE WA SOKA MKOANI TANGA.

KOCHA WA COASTAL UNION JAMES NANDWA AKITOA MAWAIDHA KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO LEO

 KOCHA MKUU WA COASTAL UNION,JAMES NANDWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO MARA BAADA YA KUMALIZIKA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YAKE NI MWADUI YA SHINYANGA.

Tuesday, December 16, 2014

“Coastal Union kukipiga na Mwadui FC ya Shinyanga Alhamisi Mkwakwani”


MABINGWA wa soka Tanzania Bara mwaka 1988 Coastal Union “Wagosi wa Kaya”inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Mwadui ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michuano wanayokabiliana nayo.


Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Alhamisi ya wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani lengo likiwa ni kukipa makali kikosi cha Coastal Union kujiwida na mechi yao ya Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison itakayochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.


Akizungumza na Coastal Union Official Site,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa mechi hiyo ni miongoni mwa michezo mbalimbali ya kirafiki wanayocheza ili kuweza kukiimarisha kikosi hicho ambacho msimu huu kimepania kufanya makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania.


El Siagi alisema kuwa timu ya Mwadau ya Shinyanga inatazamiwa kuwasili mkoani hapa Jumanne wiki hii tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkali.


Hata hiyo aliwataka wadau wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ikiwemo kuangalia wachezaji ambao wamesajiliwa msimu huu kwa ajili ya michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.


   “Tunawajua Mwadui FC sio timu mbaya hivyo naamini kutakuwa na burudani ya kukata na shoka nawasihi wakazi wa mkoa wa Tanga wajitokeza kwa wingi ili kushuhudia mchezo huo “Alisema El Siagi.


Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza mechi nyengine ya kirafiki kabla ya kutua jijini Mbeya ambapo watakwenda kucheza mechi yao ya Ligi kuu.

KOCHA WA KIUNGO MKENYA VICTOR WANYAMA ATUA COASTAL UNION,AHAIDI MAKUBWA



 Kocha Mkuu Coastal Union,James Nandwa kulia akilakiwa  na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga jana.
HAPA NI KOCHA NANGWA WA KWANZA KULIA AKIELEKEZWA JAMBO NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA KUSHOTO NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI

Kocha Mkuu Coastal Union,James Nandwa kulia akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga jana.
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
ALIYEWAHI kuwa Kocha wa Kiungo Mkenya, Victor Wanyama anayechezea soka lake kwenye klabu ya ,Southampton nchini Uingereza James Nandwa ameingia mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu ya Coastal Union ya Tanga.

Kocha huyo anachukua mikoba iliyoachwa na Kocha Yusuph Chippo aliyekwenda nchini kwao Kenya kutokana na matatizo ya kifamilia kuwa kwenye hali ambayo sio mzuri jambo ambalo lilipelekea kushindwa  kurejea nchini kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Akizungumza mara baada ya kutua jijini Tanga leo ikiwemo kulakiwa na viongozi wa klabu hivyo wakiongozwa na Meneja wake ,Akida Machai wakiwemo Katibu Mkuu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji,Kocha huyo alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo.

Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa ujio wa kocha huyo utawezesha timu hiyo kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea ya kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

Assenga amesema kuwa kutokana na uzoefu aliokuwa nao kocha huyo utawezesha kupelekea chachu kwa wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kupambana wakiwa na lengo la kuipa mafanikio timu hiyo.

Kwa upande wake,Kocha  Nandwa amesema kuwa kitu cha kwanza ni kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake iliyojiwekea ya kuwa timu bora Tanzania ili iweze kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

   “Kwanza nashukuru kupata nafasi ya kuifundisha Coastal Union nitahakikisha nitaifikisha timu hii kwenye malengo waliojiwekea ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara kutokana na uzoefu wangu niliokuwa nao “Amesema Nandwa.

Kocha Nandwa aliwahi kuzifundisha timu za soka za Harambee Stars,AFC Leopard ya Kenya pamoja na Utalii ya Kenya na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo Ubingwa wa Ligi kuu nchini humo.



Saturday, December 6, 2014

WAZEE WA KAZI Coastal Union Mazoezini


 Wachezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga wakifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Mkwakwani kujiandaa na mchezo dhini ya Prison ya Mbeya ambayo utachezwa katka uwanja wa Sokoine





Mazoezini Mkwakwani, Wanandinga wa Coastali Unioni wakijifua Mkwakwani Tanga leo asubuhi

Saturday, November 29, 2014

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA TIMU YA VIJANA YA COASTAL UNION U-20 MABINGWA WA KOMBE LA UHAI LEO KOROGWE

KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA COASTAL UNION U-20 LEO KABLA YA KUANZA SAFARI KUELEKEA WILAYANI KOROGWE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA KOROGWE UNITED

KIKOSI CHA COASTAL UNION U-20 KILICHOANZA KWENYE MECHI HIYO YA LEO NA KOROGWE UNITED,AMBAPO KABLA YA KUANZA MTANANGE HUO KULINYESHA MVUA KUBWA AMBAYO ILIPELEKEA MCHEZO HUO KUSIMAMA KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA KUENDELEA

KUSHOTO NI MKURUGENZI WA UFUNDI WA KOROGWE UNITED,FILBERT MPENZIA AKIMUELEZA KITU MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION SALIMU BAWAZIR LEO WA KWANZA KULIA NI NAIBU KADHI MKUU WA TANZANIA,SHEIKH ABUBAKARI ZUBEIR.

KIKOSI CHA COASTAL UNION KIKIPASHA KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO LEO



WALINDA MILANGO WA COASTAL UNION U-20 WAKIPASHA KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO LEO



MKURUGENZI WA BENCHI LA UFUNDI LA COASTAL UNION,MOHAMED KAMPIRA AKISISITIZA JAMBO KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO WAKATI WA MAPUMZIKO KUSHOTO NI MCHEZAJI WA ZAMANI WA COASTAL UNION NA MJUMBE WA KAMATI YA USAJILI RAZACK KAREKA LRO

MASHABIKI WA SOKA WALIOJITOKEZA KWENYE UWANJA WA SOKA CHUO CHA UALIMU KOROGWE WAKIFUATILIA MPAMBANO HUO LICHA YA KUNYESHA MVUA KUBWA

Tuesday, November 25, 2014

COASTAL UNION U-20 YAIKALISHA MONGA STARS YA VYERU WILAYANI MKINGA,YAIPIGA 1-0

KIKOSI CHA U-20 CHA COASTAL UNION KIKIPASHA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO DHIDI YA MONGA STARS AMBAPO COASTAL UNION U-20 ILIIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 BAO HILO LILIFUNGWA NA ZAMIRU ISSA DAKIKA YA 36

MAKIPA YA KIKOSI CHA U-20 COASTAL UNION WAKIPASHA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO


KOCHA WA KIKOSI CHA U-20 YA COASTAL UNION,JOSEPH LAZARO AKISISITIZA JAMBO KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO

KIKOSI CHA COASTAL UNION U-20 AMBACHO KILICHEZA NA MONGA STARS LEO NA KUWAFUNGA BAO 1-0

MWAMUZI WA MECHI HIYO,KASID KITENDO AKIWA NA WACHEZAJI WA TIMU ZOTE MBILI KABLA YA KUANZA MPAMBANO HUO

KIKOSI CHA MONGA STARS KILICHOPIGWA KIMOJA NA COASTAL UNION U-20 LEO

KOCHA WA TIMU YA VIJANA YA COASTAL UNION U-20 JOSEPH LAZARO AKISISITIZA JAMBO KWA WACHEZAJI WA TIMU HIYO LEO WAKATI WA MAPUMZIKO

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED AURORA WA PILI KUTOKA KULIA AKIFUATILIA MECHI HIYO NA VIONGOZI WENGINE WA TIMU HIYO WA KWANZA KULIA NI MENEJA WA TIMU YA COASTAL UNION AKIDA MACHAI NA KUSHOTO NI MJUMBE WA KAMATI YA USAJILI SALIM BAWAZIRI NA MWANACHAMA WA COASTAL UNION LEO


Wednesday, November 5, 2014

PICHA TANO ZA MENEJA WA COASTAL UNION AKIBADILISHA MAWAZO NA MWENYEKITI WA TANGA MIDDLE VETARAN JUZI.

MENEJA WA COASTAL UNION AKIDA MACHAI AKIBADILISHANA MAWAZO NA MWENYEKITI WA TANGA MIDDLE AGE VETERAN.



HAPA KUSHOTO NI MENEJA WA COASTAL UNION AKIDA MACHAI ALIYESIMAMA AKIZUNGUMZA JAMBO NA MENEJA WA UWANJA WA CCM MKWAKWANI ,MBWANA MSUMARI.



COASTAL UNION :MTAIPENDA MSIMU HUU.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.  

KOCHA MKUU wa Coastal Union ya Tanga, Yusuph Chippo amesema anaamini mipango ya timu hiyo ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu yatatimia na hivyo lazima watanzania lazima wataipenda.
Coastal Union ya Tanga ni timu ambayo imeanza vema msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara ambapo kwa sasa ina pointi 11 ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu.

Alisema kuwa mikakati yake ni kuhakikisha kila mechi timu hiyo inapata matokeo mazuri yatayoiwezesha kufanikisha ndoto zao kufanya mapinduzi kwenye michuano hiyo ambayo inashirikisha timu kumi na nne.

Aidha alibainisha kuwa kikubwa ambacho anajivunia ni kuwa na kikosi madhubuti ambacho kimempa dira ya mafanikio mbeleni yanayotokana na usajili mzuri ambao timu hiyo ilifanya kabla ya kuanza msimu huu.

   “Kwa hakika Coastal Hii lazima mtaipenda sasa tunajiandaa
kuwakabili wanaramaramba tukiwa na lengo moja tu la kupata pointi tatu muhimu ili kuweza kuendeleza rekodi yetu ya ushindi kama ilivyokuwa kawaida yetu “Alisema Chippo.

Akizungumzia mechi hiyo,Chippo alisema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanaendelea na mazoezi ya kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu kwa sababu hilo linawezekana kutokana na wachezaji mahiri wanaounda kikosi cha Wagosi hao wakaya.

Coastal Union itaingia kwenye mechi yao na Azam Fc mwishoni mwa wiki ikiwa na kumbukumbu ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi yao ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.