TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeanza maandalizi ya
kuelekea mechi yao na Kagera Sugar itakayopigwa
wikiendi hii kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ikiwa ni muendelezo wa Ligi
kuu soka Tanzania
bara.
Kauli hiyo ilitolewa na Kocha Mkuu wa Coastal Union,Yusuph Chippo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye
viwanja wa shule ya Sekondari Popatlaly mjini hapa.
Alisema kuwa kikosi chake kipo imara kuweza kuwavaa wakata
miwa wa bukoba kutokana na kuimarisha sehemu mbalimbali kwenye timu hiyo hasa
mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi yao
na Mgambo Shooting ambapo Coastal ilishinda bao 2-0.
Kocha huyo alisema kuwa wembe uliotumika kuwanyoa timu hiyo
ya Mgambo Shooting ndio ambao watautumia ili kuweza kupata pointi tatu muhimu
wakiwa ugenini lengo likiwa kuweza kuwa kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa
Ligi kuu .
“Tunamshukuru mungu kwa kupata pointi
tatu muhimu kwenye
mechi hii na hili linatokana na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza
kwenye mechi yetu iliyopita lakini kubwa ni umoja na mshikamano uliopo
“Alisema Chippo.
Hata hivyo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapambana vilivyo kila mchezo ili waweze kupata matokeo mazuri yatakayowawezesha kuirudishia heshima timu hiyo yenye maskani yake barabara 11 jijini Tanga.
Hata hivyo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapambana vilivyo kila mchezo ili waweze kupata matokeo mazuri yatakayowawezesha kuirudishia heshima timu hiyo yenye maskani yake barabara 11 jijini Tanga.
Katika hatua nyengine,Timu hiyo inatarajiwa kutumia usafiri
wa ndege kuelekea mkoani Kagera kucheza mechi yake ya Ligi kuu wikiendi hii
dhidi ya Kagera Sugar mechi itakayochezwa uwanja wa Kaitaba.