Friday, September 26, 2014

CHIPPO AWEKA MIPANGO YA KUCHUKUA POINTI TATU DHIDI YA MBEYA CITY KESHO SOKOINE.

 
KOCHA MKUU wa Coastal Union ya Tanga,Yusuph Chippo amesema kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi dhidi ya Mbeye City mchezo unaochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza leo ,Kocha Chippo alisema kuwa kuelekea mechi hiyo hakuna hata mchezaji mmoja ambaye ni majeruhi hivyo wana uhakika wa kuhakikisha wanapata matokea mauziri kwenye mechi hiyo.
Coastal Union iliwasilia mkoani Mbeya juzi ambapo jana ilifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa soka Polisi na uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuvaana na wapinzani wao hao.

  “Sisi tunapambana kuhakikisha matokeo mazuri yanapatikana kwa sababu hilo ndilo lengo letu kuu hii inatokana na usajili wa nguvu tulioufanya msimu huu na umakini wa wachezaji tuliokuwa nao “Alisema Chippo.
Coastal Union itavaana na Mbeya City kesho(leo) kwenye uwanja huo ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara ambapo mchezo wa kwanza ilicheza na Simba SC kwenye uwanja wa Taifa na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.


Kwa upande wake,Kocha wa makipa,Razack Siwa amesema kwenye idara yake ya walinda milango ipo imara kuhakikisha wanakuwa imara kwenye mechi hiyo.

Wednesday, September 24, 2014

CHIPPO ATAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUACHA KUANDIKAA HABARI ZA KUPIKA

Monday, September 22, 2014

HIVI NDIVYO COASTAL UNION ILIVYOIPA MCHECHETO SIMBA UWANJA WA TAIFA JANA,ZATOKA SARE YA KUFUNGANA 2-2.


KOCHA MKUU WA COASTAL UNION,YUSUPH CHIPPO AKIINGIA KWENYE UWANJA WA TAIFA JANA,KWENYE MECHI YAO DHIDI YA SIMBA
KIKOSI CHA WAGOSI WA KAYA KILICHOISUMBUA SIMBA JANA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI WA COASTAL UNION YAYO KATO LUTIMBA AKIINGIA UWANJANI HAPO JANA







BENCHI LA UFUNDI KUTOKA KULIA NI KOCHA MKUU YUSUPH CHIPPO NA KUSHOTO NI KOCHA MSAIDIZI BENARD MWALALA









Monday, September 15, 2014

JINSI COASTAL UNION WALIVYOWASILI MKOANI TANGA KUTOKEA VISIWANI PEMBA WALIPOWEKA KAMBI MWEZI MMOJA.

BEKI WA KATI WA COASTAL UNION,BAKARI MTAMA AKISHUKA KWENYE NDEGE WAKATI WAKITOKEA PEMBA.

ITUBU IMBEM GUELOR AKISHUKA KWENYE NDEGE

SHABANI KADO AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA TIMU HIYO KUWASILI MKOANI HAPA IKITOKEA PEMBA

MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAPOKEZI YA TIMU HIYO

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED AURORA WA NNE KUTOKA KULIA AKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI KUSHOTO ALBERT PETER WA KWANZA KULIA NI MENEJA WA COASTAL UNION U-20,ABDUL UBINDE.

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED AURORA AKISALIMIANA NA KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI MARA BAADA YA MAPOKEZI YA TIMU HIYO IKITOKEA PEMBA KUSHOTO NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ALBERT PETER NA KULIA NI MENEJA WA TIMU YA VIJANA YA COASTAL UNION,ABDUL UBINDE.

HAPA UMAKINI UKITAWALA.

KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI KULIA AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA WILAYA TANGA,HALIMA DENDEGO ALIYEKAA KUSHOTO


WASANII WA KUNDI LA TANGA ALL STARS WAKIWA KAZINI SAMBAMBA NA BENDI

KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI AKIZUNGUMZA NENO KABLA YA KUMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO.

KATIKATI NI MENEJA WA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO WAKIFUATILIA BURUDANI MARA BAADA YA TIMU HIYO KUFIKA KLABUNI.


ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAKIONGOZA MSAFARA KWENYE MAPOKEZI HAYO

WACHEZAJI WAKIWA WANAINGIA KAMBINI WA KWANZA KULIA NI SULEIMANI KIBUTA.

Sunday, September 14, 2014

COASTAL UNION YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR ZATOKA 1-1.

                         

TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro ikiwa ni mechi ya kirafiki kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani.

Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la kuvutia, Mtibwa Sugar ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lake lilikfungwa na Mussa Nampaka dakika ya 44.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliweza kuingia uwanjani hapo zikiwa na hari mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake.
Wakionekana kujipanga vilivyo kwenye awamu hiyo ya lala salama,Coastal Union walianza kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Mtibwa Sugar kwa dakika kadhaa hali iliyopeleka kupatikana bao la kusawadhisha lililofungwa na Itubu Imbem Guelor.

Baada ya kumalizika mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Benard Mwalala alisema mchezo huo ni kipimo tosha kwa timu hiyo kuangalia sehemu gani yenye mapungufu kabla ya kuvaana na Simba kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu.

  “Ninachoweza kusema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hii tutayafanyia kazi kwa asilimia kubwa lengo likuwa kuhakikisha tunapata matokea mazuri kwenye mechi zetu za ligi kuu “Alisema Mwalala.
Coastal Union:Gk Shabani Kado,Razack Khalifani,Hamadi Juma,Mbwana Kibacha,Yayo Kato Lutimba,Itubu Imbem Guelor,Bakari Mtama,Ramadhani Salum,Sbri Twaha,Abdallah Mfuko,Aypub Semtawa.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar:Saidi Mohamed,Hassani Ramadhani,David Luhende,Andrew Vicent,Salim Mbonde,Shabani Nditi,Ally Shomari, Mzamiru Yassin,Ame Ally,Mussa Mgosi na Mussa Nampaka.
Coastal Union walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hamadi Juma,Razack Khalfani,Yayo Lutimba na Ayoub Semtawa na kuwaingiza Amani Juma,Tumba Sued,Petro Mahundi,Obina Bright na Hussein Sued.
Nao ka upande wao,Mtibwa Sugar walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Mussa Nampaka,Mzamiru Yassin,Amme Ally na kuwaingiza Mohamed Mkopi,Hassani Mbande na Mohamed Ally.

COASTAL UNION YALAZIMISHWA SARE MTIBWA SUGAR MKWAKWANI LEO,ITUBU AFUNGA BAO

WACHEZAJI WA COASTAL UNJON YA TANGA WAKISALIMIA NA WACHEZAJI WA MTIBWA SUGAR KABLA YA KUANZA MCHEZO WAO WA KIRAFIKI LEO UWANJA WA CCM MKWAKWANI