KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Yusuph Chippo amewataka waandishi wa habari za michezo hapa nchini kuacha kupika stori kwenye vyombo vya habari badala yake waandika habari zilizokuwa na ukweli. Hatua hiyo ya Kocha Chippo inatokana na taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti moja la michezo hapa nchini likimnukuu kocha huyo kusema kuwa tatizo la Simba lipo kwenye beki na watapata wakati mgumu watakapocheza na timu ambayo inawashambuliaji wenye kasi jambo ambalo hakulisema. Chippo alisema kuwa kitendo hicho kimemshangaza sana kuona waandishi wanaacha kufanya kazi zao kwa ueledi mkubwa kwa lengo la kuchochoea kasi ya maendeleo ya soka nchini badala yake wamekuwa wamekuwa wakitunga stori ambazo hazipo. Alisema kubwa zaidi lililomshangaza ni kuona taarifa hiyo ikiandika kuwa alisema kwa jinsi Simba inavyocheza itapata wakati mgumu itakapocheza na Yanga, kiungo na washambuliajio wako vizuri lakini beki yao ina tatizo hivyo wanahitaji kuangalia kwa umakini hasa washambuliaji wa kasi. Aidha alisema habari hizo hazifahamu wala hakuzungumza na mwandishi wa aina yoyote ile hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo kwani wanatengeneza masuala yasiyokuwa mazuri kwenye jamii hususani ya wanamichezo hapa nchini. “Tunafahamu kuwa waandishi wa habari wanakazi kubwa sana ya kuielimisha jamii inayowazunguka hivyo nawasihi fanyeni kazi zetu kwa ueledi mkubwa na kuacha kupika stori kwenye vyombo vyenu “Alisema Chippo. Hata hiyo alisema timu hiyo imeanza kuipiga mahesabu ya kuhakikisha inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania bara itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya. Chippo alisema kuwa kikosi chake kimekuwa na hari mpya hivyo atahakikisha anawaanda vizuri wachezaji wake ili waweze kucheza kandanda nzuri ambalo linawawezesha kupata mabao mengi kwenye mechi hiyo. Coastal Union tayari imekwisha kuwasili mkoani Mbeya ikijiandaa na mechi yake dhidi ya Mbeya City itakayochezwa kwenye uwanja wa sokoine mkoani humo. Mwisho. |
Wednesday, September 24, 2014
CHIPPO ATAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUACHA KUANDIKAA HABARI ZA KUPIKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment