Thursday, September 11, 2014

MECHI YA COASTAL UNION NA MTIBWA SUGAR YASOGEZWA MBELE SASA KUCHEZWA JUMAPILI



NA MWANDISHI WETU, TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga “Wagosi wa Kaya” ambayo ilikuwa ichezwa Jumamosi wiki hii imesogozwa mbele sasa kucheza Jumapili mchezo wa kirafiki na timu ya  Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara ambao unatarajiwa kuanza Septemba 20 hapa nchini.
Mchezo huo umesogezwa mbele kwa sababu ya kuwepo kwa mechi za uingereza Jumamosi
Akizungumza leo, Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na tayari walishafanya mazungumzo na uongozi wa wakata miwa hao hivyo watawasili mkoani hapa siku moja kabla ya mchezo huo.
Assenga amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa timu ya Coastal Union kucheza ikiwa mkoani hapa baada ya kurejea kutoka Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi ya mwezi mmoja kwa ajili ya matayarisho ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Amesema baada ya mchezo wa kwanza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Morogoro hivyo waliona umuhimu wa mechi hiyo lengo likiwa kukipa makali kikosi hicho kabla ya kuwavaa wekundu wa msimbazi Simba siku ya ufunguzi wa Ligi kuu.
Ameongeza kuwa wanategemea mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa sana hivyo wakazi wa Tanga na vitongoji vyake watumia fursa hii kuja kuiona timu yao ya Coastal Union ikipambana kwenye mchezo huo kabla haijaanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara
Hata hivyo amesema kuwa msimu huu timu hiyo imepania kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi zake za nyumbani na ugenini ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara .
Mwisho.

No comments:

Post a Comment