TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga leo
imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro ikiwa ni
mechi ya kirafiki kuelekea maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara
mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani
mkubwa kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri
na la kuvutia, Mtibwa Sugar ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lake
lilikfungwa na Mussa Nampaka dakika ya 44.
Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda
mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliweza
kuingia uwanjani hapo zikiwa na hari mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa
baadhi ya wachezaji wake.
Wakionekana kujipanga vilivyo kwenye awamu hiyo ya
lala salama,Coastal Union walianza kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni
mwa Mtibwa Sugar kwa dakika kadhaa hali iliyopeleka kupatikana bao la
kusawadhisha lililofungwa na Itubu Imbem Guelor.
Baada ya kumalizika mchezo huo, Kocha Msaidizi wa
Coastal Union,Benard Mwalala alisema mchezo huo ni kipimo tosha kwa timu hiyo
kuangalia sehemu gani yenye mapungufu kabla ya kuvaana na Simba kwenye mechi ya
ufunguzi wa Ligi kuu.
“Ninachoweza
kusema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hii tutayafanyia kazi kwa asilimia
kubwa lengo likuwa kuhakikisha tunapata matokea mazuri kwenye mechi zetu za
ligi kuu “Alisema Mwalala.
Coastal Union:Gk Shabani Kado,Razack
Khalifani,Hamadi Juma,Mbwana Kibacha,Yayo Kato Lutimba,Itubu Imbem
Guelor,Bakari Mtama,Ramadhani Salum,Sbri Twaha,Abdallah Mfuko,Aypub Semtawa.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar:Saidi Mohamed,Hassani
Ramadhani,David Luhende,Andrew Vicent,Salim Mbonde,Shabani Nditi,Ally Shomari,
Mzamiru Yassin,Ame Ally,Mussa Mgosi na Mussa Nampaka.
Coastal Union walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hamadi
Juma,Razack Khalfani,Yayo Lutimba na Ayoub Semtawa na kuwaingiza Amani
Juma,Tumba Sued,Petro Mahundi,Obina Bright na Hussein Sued.
Nao ka upande wao,Mtibwa Sugar walifanya mabadiliko
kwa kuwatoa Mussa Nampaka,Mzamiru Yassin,Amme Ally na kuwaingiza Mohamed
Mkopi,Hassani Mbande na Mohamed Ally.
No comments:
Post a Comment