KOCHA MKUU wa Coastal Union ya Tanga,Yusuph Chippo amesema
kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi dhidi ya
Mbeye City mchezo unaochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza leo ,Kocha Chippo alisema kuwa kuelekea
mechi hiyo hakuna hata mchezaji mmoja ambaye ni majeruhi hivyo wana uhakika wa
kuhakikisha wanapata matokea mauziri kwenye mechi hiyo.
Coastal Union iliwasilia mkoani Mbeya juzi ambapo
jana ilifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa soka Polisi na uwanja wa Sokoine
mkoani Mbeya ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuvaana na wapinzani
wao hao.
“Sisi
tunapambana kuhakikisha matokeo mazuri yanapatikana kwa sababu hilo ndilo lengo
letu kuu hii inatokana na usajili wa nguvu tulioufanya msimu huu na umakini wa
wachezaji tuliokuwa nao “Alisema Chippo.
Coastal Union itavaana na Mbeya City kesho(leo)
kwenye uwanja huo ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara ambapo
mchezo wa kwanza ilicheza na Simba SC kwenye uwanja wa Taifa na kutoka sare ya
kufungana mabao 2-2.
Kwa upande wake,Kocha wa makipa,Razack Siwa amesema
kwenye idara yake ya walinda milango ipo imara kuhakikisha wanakuwa imara
kwenye mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment